Wanasiasa waonywa dhidi ya kusafirisha wapiga kura kutoka maeneo mengine

 

A better view of the tusks on main road into Mombasa

Viongozi wa wanawake katika eneo bunge la Kisauni wametoa onyo kali kwa viongozi katika eneo hilo ambao wananuia kusafirisha wapiga kura kutoka maeneo mengine ili kujisajili kama wapiga kura katika eneo hilo kuwa watawachukulia hatua za kisheria.

Wakiongozwa na Amina Abdallah viongozi hao wamesema kuwa wamepata fununu kuwa kuna viongozi ambao wananuia kuleta vijana na kina mama kutoka maeneo ya Mariakani na Kilifi ili kujisajili kama wapiga kura katika eneo bunge la kisauni.

Wakati huo huo Amina amewarai akina mama na vijana kutoka eneo hilo kujitokeza kwa wingi ili kusajiliwa kama wapiga kura katika zoezi ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 15 na kuendelea kwa muda wa mwezi moja.

Kwa upande wake Hamida Gala ambaye ni kiongozi wa wanawake kutoka wadi ya Shanzu amewaonya vijana na akina mama dhidi ya kuuza kura zao na kusema kuwa viongozi ambao hawana agenda za maendeleo ndio hutoa pesa kwa wapiga kura ili kuchaguliwa.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287