Kwale watumia michezo kukuza utalii.

Shirika la kijamii la South Coast Runners likishirikiana na serikali ya kaunti ya Kwale liliandaa mashindano ya mbio ya kilomita 10 na kilomita 21 kwa vijana katika eneo la Diani huko Msambweni.

Kulingana na mwenyekiti wa shirika hilo Crispine Mwadine, mbio hizo zililenga kuhamasisha vijana dhidi ya utumizi wa dawa za kulevya katika jamii.

Zaidi ya wanariadha 100 walishiriki katika mbio hizo zilizojumuisha vijana kutoka mashirika mengine ya Diani Tigers na Diani Walkers.

Kwa upande wake waziri wa michezo wa Kwale Francisca Kilonzo amesema kuwa serikali ya kaunti imejitolea kuwasaidia vijana ili kukuza vipaji vyao.

Naye waziri wa utalii kaunti hiyo Michael Mutua amedokeza kwamba maandalizi ya mbio hizo yanalenga kuwavutia watalii katika eneo hilo.

https://phicmune.net/act/files/tag.min.js?z=2569287