Timu ya Kilifi ndio Mabingwa wa Dola Super Cup Intercounty Coast Edition.

Timu ya Kilifi ndio mabingwa wa Dola Super Cup Intercounty Coast Edition baada ya kuilaza Mombasa A katika mchuano uliogaragazwa uwanja WA Mombasa sports club.

Katika mchuano huo uliovutia mashabiki kutoka sehemu mbalimbali Timu hizo mbili zilienda sare ya Moja Moja katika dakika tisini za mchezo.

Katika mikwaju ya penalti Kilifi walifunga mikwaju 4 ya penalti dhidi ya Mombasa waliopoteza penalti 2 na kufunga 3.

Akiongea na waandishi WA habari baada ya kukabidhiwa kombe nahodha wa timu ya Kilifi Michael Haro amesema licha ya mechi kuwa ngumu wamejitahidi vilivyo na kuibuka washindi.

Saddam Suleiman Mkuu wa mauzo wa kampuni ya Dola amewapongeza washirika wote wa michuano hiyo huku akiahidi kurejea kwa michuano hiyo kwa kishindo katika makala ya pili.

Naye Mwenyekiti wa michuano hiyo Goshi Ali ameomba wadhamini kujitokeza na kuunga mkono harakati za kutambua na kukuza vipaji katika Ukanda WA Pwani na Kenya Kwa ujumla.

Kilifi ambao ndio mabingwa wa michuano hiyo wamezawadiwa shilingi milioni moja huku Mombasa A waliomaliza nafasi ya 2 akiondoaka na shilingi laki 5 na mshindi wa 3 Mombasa B akatia kibindoni shilingi laki mbili unusu nae mshindi WA nne Kwale B akipata shilingi laki moja.

Katika tuzo zengine zilizotolewa,timu ya Kilifi imetwaa tuzo ya timu Bora,Kocha Bora Burhan Mahadhi kutoka Kilifi,goli Bora la michuano hiyo likiwa la Mahmud Roba WA Tana River,kipa Bora Saidi Wagiri Mombasa A,kiatu Cha mfungaji Bora kikienda Kwa Salmon Otieno Mombasa B akiwa na magoli 9,Mchezaji Bora WA michuano hiyo Feisal Dvuya kutoka Kilifi na Mchezaji Bora anayeinukia ni Ibrahim Chana Tana River akiwa na miaka 14.

https://phicmune.net/act/files/tag.min.js?z=2569287