Mradi wa Seneta Miraj wa kustawisha kina mama na vijana awamu ya pili wangoa nanga.

Kina mama katika eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa wamepokea mafunzo maalum ya kuwawezesha kudhibiti mapato yao na kujiwekea akiba kupitia akaunti za benki kwa manufaa ya siku za usoni.

 

Katika hafla hiyo ya uwezeshaji wa kina mama inayofahamika kama STAWISHA EMPOWERMENT PROGRAM iliyoandaliwa na wakfu wa MAMA HAKI,Seneta Maalum Miraj Abdillah amewarai kina mama hao kukumbatia mifumo ya kisasa kuwekeza kwenye biashara na kuweka akiba ili kujikomboa na umaskini.

Miraj akiwataka kina mama hao kufanya biashara kwa malengo ambayo yatawaletea natija za kudumu katika maisha yao.

Aidha Miraj amesema kupitia wakfu wake atawafungulia wamama hao sacco ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata pesa za ruzuku kutok kwa serikali kila mwaka sawia na kuweka pesa zao katika mikono salama.

Vevile seneta Miraj amewataka kina mama hao kuripoti visa vya dhulma za kijinsia dhidi yao na watoto kwa idara husika ili wahusika kuchukuliwa hatua badala ya kutatua visa hivyo kinyumbani.

Hii ni awamu ya pili ya mradi wa STAWISHA EMPOWERMENT PROGRAM wakfu wa MAMA HAKI unapania kufikia Vijana na kina Mama 10,000 katika Kaunti ya Mombasa ikiwa ni azma ya Miaka 5 yakuwapa Elimu ya kifedha, uwekezaji, utaalamu wa kidijitali, mbinu za kukuza Biashara, ujasiriamali na ujuzi utakaowezesha kuendeleza Biashara zao.