Isaack Hassan aitaka wizara ya fedha kuongeza pesa ili kufanikisha shughuli ya usajili wa wapiga kura

download (7)

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan sasa amewarai magavana kuingilia kati na kutoa msaada wa fedha ili kuwezesha tume hiyo kuwasajili wapiga kura wapya kote nchini.

Hassan amesema tume hiyo ina upungufu wa zaidi ya shilingi bilioni moja na kutaka wizara ya fedha kuongeza pesa zaidi.

Magavana kwa upande wao wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la magavana Peter Munya, wamepinga ombi hilo wakisema kuwa ni sharti serikali kuu ifadhili zoezi hilo kama ilivyo kwenye katiba.

Munya amesema kuwa katiba haiwaruhusu magavana kutoa mgao wa fedha walizopewa kufadhili shughuli hiyo.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287