Baadhi ya viongozi waunga mkono hatua ya rais ya kupunguza marupurupu

images (3)

Siku moja tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kusema kuwa watapunguza marupurupu ya viongozi serikalini ili kupunguza gharama ya serikali baadhi ya wabunge wamejitokeza na kuunga mkono hatua hiyo.

Mbunge wa Mvita, Abdulswamad Sharrif Nassir amesema kuwa anaunga mkono hatua hiyo japo wangependa serikali kueleza jinsi pesa hiyo itakavyotumika.

Hapo jana rais Uhuru alisema kuwa watapunguza marupurupu ya usafari ya viongozi kwa asilimia 50.

Miongoni mwa viongozi ambao wataathirika na hatua hiyo ni majaji, wabunge, magavana ,Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.