Moto mkubwa wazuka Mombasa katika kampuni ya Solvochem East Africa

Ca7-a11W0AACUzL

Mali ya mamilioni ya fedha imeharibika baada ya moto mkubwa kuzuka katika kampuni ya Solvochem East Africa eneo la Shimanzi kaunti ya Mombasa.

Walioshuhudia wamesema kuwa moto umeanza mwendo wa saa tisa alasiri lakini maafisa wa zima moto kutoka serikali ya Mombasa wamefanikiwa kuuzima.

Chimbuko la moto huo lingali kujulikana huku ikihofiwa kuwa huenda moto huo umesababishwa na hitilafu za umeme.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287