Wakaazi katika shamba lililokuwa la Waitiki kupata afueni

download (11)

Huenda wakaazi wa Likoni wanaoishi katika shamba lililokuwa la Waitiki wakapata afueni baada ya gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho kuahidi kuwalipia ada za hati miliki wanazotozwa wakaazi hao.

Akihitubia mkutano wa siasa za uchaguzi mdogo wa Malindi gavana huyo amesema kuwa wengi wa maskwota hao ni walala hoi, hivyo ni jukumu la serikali yake kuwashughulikia wakaazi wake vilivyo.

Mapema mwaka huu rais Uhuru Kenyatta aliongoza zoezi la utoaji wa hati miliki kwa wakaazi hao wa Likoni, ila ikasisitiza kuwa ni sharti kila mmoja wao alipe ada ya shilingi alfu 180 ili kuwa mmiliki halisi wa ardhi hiyo.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287