Kavuludi akana madai ya ufisadi katika tume ya huduma kwa polisi

images (6)

Mwenyekiti wa tume ya huduma kwa polisi Johnstone Kavuludi amepuuzilia mbali madai kuwa tume hiyo inajihusisha na ufisadi huku akisema kuwa maisha ya makamishina wa tume hiyo yamo hatarini kwa kutishiwa maisha kila uchao.

Kavuludi amesema kuwa wamepokea barua ambayo haikubainisha yule aliyeituma ikimtishia Kavuludi na makamishina kuhusu zoezi la mchujo, barua wanadai kuwa huenda imetoka kwa maafisa waliofeli kwenye zoezi lililopita.

Makamishina hao wamesisitiza kuwa zoezi hilo litaendelea licha ya vitisho hivyo. Amekana madai kuwa tume hiyo hupokea hongo kutoka kwa maafisa wa polisi wa ngazi ya juu ambao watafanyiwa mchujo akisema huenda kuna matapeli ambao hudanganya maafisa hao kutoa hongo kwa kigezo kuwa watapitishwa katika zoezi hilo.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287