Taarifa kutoka mahakamani Mombasa

New-Jersey-personal-injury-law-firm-300x300

Maafisa wawili wa polisi walioshtakiwa katika mahakama ya Mombasa kwa kosa la mauaji ya msichana wa umri wa miaka 14 mwaka wa 2014 katika kijiji cha Maweni kaunti ya Kwale leo wamepatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.

Akitoa uamuzi wake ,Jaji Martin Muya amesema kuwa ingawa washtakiwa hao walikanusha shtaka hilo lakini ushahidi uliotolewa mbele ya mahakama umedhibitisha wazi kuwa washtakiwa ndio waliotekeleza mauaji hayo.

Washtakiwa Veronicah Gitahi na Issa Mzee wanadaiwa kutenda kosa hilo katika kijiji cha Maweni wilayani Kinango kaunti ya Kwale mnamo tarehe 22 mwezi Agosti mwaka 2014.

Jaji Muya ameongeza kuwa atatoa uamuzi wake wa mwisho dhidi ya washtakiwa hao mnamo tarehe 12 mwezi huu wakati kesi hiyo itakapotajwa na hatma yao kujulikana.

Na katika mahakama hiyo….

Mwanamume wa umri wa miakaa 39 anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji ya mzee wa umri wa miaka 65 katika eneo la Samburu wilayani Kinango kaunti ya Kwale amehukumiwa kifo kwa kosa hilo.

Mshtakiwa Elisha Mwarua amepewa adhabu hiyo na jaji Martin Muya baada ya kumpata na hatia kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi pamoja na upande wa serikali.

Shtaka dhidi yake ni kuwa mnamo tarehe 24 mwezi Agosti mwaka 2014 katika eneo la Samburu wilayani Kinango kaunti ya Kwale kinyume cha sheria alimuua Tsuma Tsimba.

https://yonhelioliskor.com/act/files/tag.min.js?z=2569287