Mamlaka ya mpito yafika mbele ya bunge la kitaifa

images (5)

Mamlaka ya mpito imefika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa ya utekelezaji katiba, ili kusihi kupewa muda zaidi wakuhudumu.

Mwenyekiti wa TA Kinuthia Wamwangi amesema iwapo mamlaka hiyo italazimika kufungasha virago Machi 4 kuambatana na katiba basi ,mfumo wa ugatuzi utakuwa hatarini.

Ameeleza hofu kuwa hadi sasa wapo wafanyikazi wengi wa serikali kuu ambao wangali kuhamishwa hadi serikali za ugatuzi huku wengine waliohamishwa wakiwa wanatishiwa kufurushwa kazini.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati hiyo Njoroge Baiya amesema kamati hiyo japo haijaridhishwa ni kwa nini TA inahitaji muda zaidi, ameahidi kamati yake itawasilishwa ripoti yake bungeni kuhusu swala hilo.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287