Mkurugenzi mkuu wa KPA asimamishwa kazi

Gichiri-Ndua

Mkurgenzi mkuu wa mamlaka ya bandari ya Mombasa KPA Gichiri Ndua amesimamishwa kazi kwa muda ilikutoa nafasi ya uchunguzi unaondelea kuhusu maswala ya ufisadi yanayokabili bandari hiyo.

Hatua hii imechukuliwa na waziri wa uchukuzi James Macharia kwa kutilia maanani pendekezo la bodi ya bandari ya KPA kuwasimamisha viongozi wakuu katika bandari hiyo ikiwemo wakuu wa usalama.

Aidha katika kikao na waandishi wa habari waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery amewaonya wafanyibiashara wanaotumia bandari hiyo kuingiza mizigo yao bila kulipa ushuru kuwa serikali itawakabili kupitia mkono wa sheria.

Katika mabadiliko hayo kamishna mkuu wa mamlaka ya ukusanyaji ushuru na kutoza kodi KRA John Njiriaini ameeleza kuwa mamlaka hiyo imeanza mikakati ya kutangaza wazi nafasi ya kuajiriwa afisa mkuu wa kuajiri wafanyikazi KRA ili kurudisha nidhamu kwa wafanyikazi ambao hivi karibuni wengi wao wamehusishwa na visa vya ufisadi katika shughui za ukaguzi wa bidhaa katika bandari hiyo.

Zaidi ya maafisa 50 wa KRA waliokuwa wakihudumu katika badandari ya KPA wamepewa uhamisho kutoka Mombasa hadi sehemu nyengine humu nchini kama njia moja wapo ya kinidhamu.

https://yonhelioliskor.com/act/files/tag.min.js?z=2569287