Wagombea wa CORD na JAP waidhinishwa na IEBC

charo-pic

Wagombe wa kiti cha eneo bunge la Malindi kupitia chama cha JAP na muungano wa CORD wameidhinishwa na IEBC ili kushiriki uchaguzi huo mdogo.

Wily Mtengo wa chama cha ODM na ambaye pia masomo yake yalitiliwa shaka alikuwa ameandamana na viongozi wakuu wa chama hicho.

Naye mgombea wa kiti hicho kwa chama cha Jubilee Philip Charo ameandamana na viongozi kadhaa kuhakikisha anaidhinishwa rasmi kama mgombea.

Wagombea 10 tayari wamejitokeza kuwania kiti hicho baada ya aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Dan Kazungu Kambi kuteuliwa  kuwa waziri wa madini.

 

 

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287