Uhalifu wakithiri Nyali

Police-Tape-Stock-Image_1439676922379_107286_ver1.0

Visa vya uhalifu vimeonekana kuongezeka katika eneo bunge la Nyali baada ya mali yenye thamani isiyojulikana kuripotiwa kupotea katika duka la kuuza bidhaa za kielektroniki eneo la freretown,usiku wa kuamkia leo.

Hii ni baada ya watu wasiojulikana kulivamia duka hilo na kuvunja milango na kuingia ndani na kisha kutekeleza uhalifu huo.

Mmiliki wa duka hilo Charles Karoni amewaambia waandishi wa habari kuwa watu hao walichukua hatua hiyo baada ya kutofungua duka hilo hapo jana.

Sasa wakaazi wa eneo hilo wameitaka idara ya usalama kuongeza doria katika eneo hilo nyakati za usiku.

https://yonhelioliskor.com/act/files/tag.min.js?z=2569287