Keter aikashifu vikali EACC

Kimages (3)

Huenda maafisa wakuu wa tume ya kupambana na ufisadi nchini EACC wakapigwa msasa upya ,iwapo mswada utakaowasilishwa bungeni kesho na mbunge wa Nandi Alfred Keter utapitishwa.

Keter amekashifu vikali tume ya EACC baada ya tume hiyo kumuondelea lawama aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru kuhusu kashfa ya NYS ,huku akisisitiza kuwa hakuna uchunguzi wowote uliotekelezwa.

Mbunge huyo vilivile ametilia shaka mbinu ya tume ya EACC kumfanya Anne Waiguru shahidi mkuu kwenye kashfa hiyo ambapo pia yeye ni mhusika.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287