Wataalamu wa kike walaani vikali likizo ya lazima ya Sumaya Uthman

sumayya hassan-athmani

Wataalamu wanawake wakiislamau wamejitokeza na kulaani hatua ya kupewa likizo ya lazima kwa afisa mkuu mtendaji wa shirika la mafuta nchini Kenya  Sumaya Uthman  na kumtaka rais Uhuru Kenyatta na waziri wa kawi Charles Keter kumregesha kazini mara moja.

 

Wakiongozwa na mbunge mteule Zulekha Juma akina mama hao wamesema ni sharti Sumaya aregeshwe mamlakani ili amalize awamu yake na aendelee kuwa hudumia wa Kenya na kulipatia manufaa taifa hili.

Hata hivyo wamesema iwapo Sumaya alitenda makosa yanayolazimisha yeye kupewa likizo ya lazima basi hatua kama hiyo ingechukuliwa na bodi ya shirika hilo.

Kulingana na mwanachama wa baraza la shura nchini Fatma Hydar amesema kumekuwa na hulka ya kuwapiga vita wanawake wanao ongoza mashirika ya kiserikali huku mara nyingi wakiondolewa mamlakani bila mbinu mwafaka kuchukuliwa.

Fatma ametowa wito kwa mwenyekiti wa tume ya usawa na jinsia Winfred Lichuma kuliangazia swala hilo na kuhakisha kuwa sheria ya thuluthi mbili inatekelezwa kikamilifu ili kuepusha wanawake kuendelea kunyanyaswa.

Aidha amesema kuwa licha ya wanawake nchini Kenya kuwa nusu ya idadi ya jumla ya watu humu nchini bado hawapati nafasi kuu za uongozi na zile chache walizozipigania bado wanapigwa vita kunyang’anywa jambo ambalo anasema linatishia uchumi wa taifa la kenya.

 

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287