Uhuru atarajiwa kuongoza ufunguzi wa kanisa Kisumu

images (5)
Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuzuru kaunti ya Kisumu ili kuongoza hafla ya ufunguzi wa kanisa moja katika ngome hiyo kuu ya kinara wa CORD Raila Odinga.
Rais anatarajiwa kufungua rasmi kanisa hilo la Seventh Day Adventist eneo la Mambo leo, wakati ambapo mpinzani wake Raila Odinga ataongoza msafara wa CORD hadi mjini Malindi kaunti ya Kilifi kufanya kampeni za kutafutwa uungwaji mkoni dhidi ya mgombea wao Willy Mtengo.
Hii itakua ziara ya 6 ya Uhuru mjini Kisumu tangu kuchaguliwa kwake na hafla 3 ya ufunguzi wa makanisa nchini.
Wakati huo huo……… Huwenda mrengo wa CORD ukajipata nje ya kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi mdogo wa Malindi kufuatia madai kuwa Willy Mtengo anamiliki stakabadhi ghushi za shule.
Hatua hii itakua pigo kubwa kwa CORD ambapo wanaimani kubwa ya kunyakua kiti hicho kilichowachwa wazi baada ya mbunge Dan kazungu kuteuliwa kuwa waziri wa Madini.
https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287