JSC yapendekeza kuteuliwa jopo la kumchunguza zaidi Tonui

140805171537-qmb-africa-terrorism-uhuru-kenyatta-intv-00014423-horizontal-gallery

Tume ya huduma za mahakama imependekeza rais Uhuru Kenyatta kuteuwa jopo ili kumchunguza zaidi, jaji Philip Tonui kuhusu sakata ya rushwa ya shilingi milioni mia mbili.

Mwenyekiti wa JSC jaji mkuu Willy Mutunga amesema kuwa kamati iliyotwikwa jukumu la kumchunguza imegundua kuwa palikuwa na mawasiliano ya kisiri kati ya jaji huyo na gavana Evans Kidero.

Mutunga amesema kuwa licha ya kuwa palikuwa na mawasiliano kunahaja ya kuundwa kwa jopo hilo ili kuchunguza madai hayo kwa kina zaidi.

Hatahivyo gavana wa kaunti ya Nairobi Evans Kidero amepinga vikali madai hayo kuwa alitoa rushwa ya shilingi milioni mia mbili ili kumshawishi jaji huyo kutupilia mbali kesi iliyowasilishwa mahakamani humo na Ferndnand Waititu baada ya uchaguzi.

Kwa upande mwengine baadhi ya viongozi wa kisiasa wanamtaka jaji mkuu Willy Mutunga kijiuzulu kutokana na kuongezeka kwa tuhuma za ufisadi katika idara ya mahakama.

Ikiwa tume hiyo maalum itampata na hatia jaji huyo basi hatakuwa na budi ila kuondolewa katika huduma na mahakama na kuwa jaji wakwanza wa mahakama ya juu kuachishwa kazi kutokana na rushwa.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287