Mitandao kutumika katika kufuatilia uwajibikaji wa viongozi

Auditor-General-Edward-Ouko

Mkaguzi mkuu Edward Ouko ametangaza mpango wa kutumia mitandao ya kijamii katika kuhakikisha wakenya wanashiriki katika maswala ya uwazi na uwajibikaji dhidi ya viongozi.

Akizungumza na wanahabari katika warsha ya uhamasiho mjini Naivasha, Ouko amesema kuwa watatumia umaarufu na ukuaji wa teknologia kuwapa motisha wakenya kufuatilia na kuripoti taarifa kuhusu utumiaji mbaya wa mali ya umma, pamoja na kudorora kwa miradi ya maendeleo iliyofadhiliwa na serikali.

Mkaguzi huyo ameongeza kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa watu binafsi pamoja na mashirika yaliyopewa kandarasi hizo, wanawajibika katika kazi zao pamoja na kurahisha kufuatilizia miradi hiyo ya kaunti na serikali kuu.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287