Hisia kuhusu tarehe ya uchaguzi mkuu zaibuka

Aden-Dualeh
Hisia mseto kuhusu tarehe ya kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017 zinazidi kuibuka miongoni mwa viongozi nchini.
Spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi ameonya kuwa huenda tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ikapata shida iwapo uchaguzi huo utaandaliwa Jumanne ya pili ya mwezi Agosti kwani bunge litakua limevunjwa na bajeti haitaweza kuidhinishwa kuendesha uchaguzi.
Amesema iwapo wananchi watapiga kura mwezi huo basi itabidi bajeti ya mwaka ujao ijadiliwe na kuidhinishwa ifikapo mwezi Aprili kabla ya bunge kuvunja vikao vyake ili kuenda kusaka kura za kurudi tena bungeni.
Hata hivyo kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale amekanusha kwamba IEBC itakosa fedha za kufanikisha uchaguzi huo akisema bajeti itapitishwa kwa wakati ufaao ili vikao vitakapohairishwa fedha zitakua zimetengwa tayari.
https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287