Wahudumu wa taxi waipa serikali siku 7 kuondoa kampuni ya taxi ya Uber

1288260

Wahudumu wa taxi jijini Nairobi wameipatia serikali makataa ya siku saba kuondoa kampuni ya huduma za taxi ya Uber la sivyo watasitisha shughuli za usafiri jijini humo.

Katika kikao na waandishi wa habari mwenyekiti wa muungano wa wahudumu wa taxi, Mwangi Mubia wamekashifu vikali wahudumu wa Uber wakidai kuwa wamekuwa wakishambulia wahudumu wengine.

Wahudumu hao wanasema kuwa tayari wameandikia barua idara ya polisi kuhusu swala hilo huku wakisema kuwa kampuni ya Uber imekuwa ikiongeza nauli kila uchao bila ya kushauri wahudu hao.

Haya yanajiri huku wahudumu wa wawili wa taxi wakitarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kushukiwa kumshambulia mhudumu mmoja wa kampuni ya Uber mtaani Kileleshwa.

Makao makuu ya polisi tayari yamedhibitisha kuwa wanaendelea na uchunguzi kuhusu swala hilo. MWAURA

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287