Kamati iliyoundwa kuchunguza ufisadi dhidi ya Tonui kuwasilisha ripoti Ijumaa

image316

Kamati maalum iliyoundwa ili kuchunguza madai ya ufisadi dhidi ya jaji Phillip Tonui imesema kuwa itawasilisha ripoti yake siku ya Ijumaa kinyume na ilivyotarajiwa hii leo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Margret Kobia ameambia waandishi wa habari kuwa kamati hiyo ingali inatathmini mapendekezo yake kabla ya kuiwasilisha.

Hapo jana kamati hiyo ilimdadisi gavana wa Nairobi Evans Kidero ambaye anadaiwa kumpa hongo jaji huyo ya shilingi milioni mia mbili ili kutulipilia mbali kesi ya uchaguzi.