Michael Kamau atakiwa kufika mahakamani kwa madai ya kuenda kinyume na sheria za kifedha za serikali

0465Transport-Cabinet-Secretary-Michael-Kamau

Mahakama moja jijini Nairobi imemtaka aliyekuwa waziri wa uchukuzi na miundo msingi mhandisi Micheal Kamau kufika mahakamani hapo kesho bila kufeli kwa ajili ya kuskizwa kwa kesi yake inayodai kuwa alienda kinyume na sheria za serikali za kifedha.

Kamau hakufika mahakamani hii leo kwa sababu za kiafya swala lililo pelekea upande wa mshtaka kuwasilisha ombi la kutaka kukamatwa kwake.

Hata hivyo ombi la kutaka kukamatwa kwake limekataliwa na mahakama hiyo na badala yake kutowa wito wamkutaka afike mahakamani hapo kesho.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287