Kidero aunga mkono usajili wa NYS kwa njia ya elekroniki

 

images (3)

Gavana wa kaunti ya Nairobi Evans Kidero amesema kuwa aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru alianzisha miradi ya NYS jijini humo ili kujinufaisha kisiasa.

Kidero amesema kuwa miradi hiyo imekosa kufaidi vijana katika vitongoji vya jiji hilo kutokana na kuingizwa mkono wa siasa.

Hatahivyo ameunga mkono hatua ya serikali kusajili vijana wa NYS kupitia njia ya electroniki akisema kuwa itawasaidia kunufaika na mishahara.

Baadhi ya viongozi jijini Nairobi wamemshinikiza Waiguru kuwania ugavana, lakini amesema kuwa yuko katika juhudi za kushauriana na washikadau kabla ya kutangaza rasmi.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287