GSU washika doria nje ya Portlink na Portside Mombasa

kisaunimpaliha_0

Maafisa wa kukabiliana na ghasia wanaendelea kushika doria nje ya kampuni mbili zilizofungwa mjini Mombasa na ambazo zinahusishwa na familia ya gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho.

Afisa mkuu wa polisi  bandarini Zakayos Ngeno amewaambia waandishi wa habari kuwa wamepokea amri hiyo kutoka kwa inspekta generali wa polisi Joseph Boinet kufunga kampuni hizo mara moja.

Ngeno ameongeza kuwa wangali wanaendelea na uchunguzi kuhusu kampuni hizo baada ya shirika la KRA nchini kuagiza kufungwa kwa muda usiojulikana.

Kufungwa kwa kampuni hizo za Portlink na Portside kumezua hisia kali huku viongozi wa upinzani wakikashifu serikali wakidai inakandamiza viongozi wa upinzani.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287