Malori ya WHO yakamatwa Mandera

Convoy

Malori matatu yanayomilikiwa na shirika la chakula duniani yamekamatwa kaunti ya Mandera,kwa madai ya kuwasafirishia chakula wapiganaji wa Al Shabab.

Kamishna wa kaunti ya Mandera Fredrick Shisia akithibitishia tukio hilo amesema malori hayo yalikuwa yanaelekea Dhola Somalia kabla kukamatwa.

Amesema kuwa serikali imebidi kuchukua msimamo huo kwa kuwa haina nia ya kuwafadhili Al Shabab kisha wageuke kuendelea kutishia usalama nchini.

Serikali ya Kenya sasa imesema inastahili kupata maelezo rasmi kutoka kwa shirika hilo ya kusema ni nani haswa anaenufaika na chakula hicho.

https://yonhelioliskor.com/act/files/tag.min.js?z=2569287