Kidero atishia kumchukulia hatua yeyote atakaemhusisha na kashfa ya rushwa

1015908_0

Gavana wa kaunti ya Nairobi Dakta Evans Kidero ametishia kumchukulia hatua za kisheria yeyote ambaye atamhusisha na kashfa ya rushwa kwa jaji wa mahakama ya juu zaidi nchini Philip Tunoi.

Akizungumza baada ya kufika mbele ya kamati maalum inayochunguza madai hayo Kidero amesema kuwa tuhuma hizo zinalenga kumchafulia jina.

Kidero hata hivyo amesema kuwa hajawahi kukutana ana kwa ana na jaji huyo lakini yeye humtizama kwa runinga tu.

Hapo jana kamati hiyo ilimdadisi jaji Tonui ambaye anadaiwa kupokea shilingi milioni mia mbili ili kutupilia kesi dhidi ya gavana huyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2013.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287