Oparesheni kuwasaka Al Shabaab yaendelea Lamu

1

Maafisa wa KDF wanaendelea na oparesheni yao ya kukabiliana na wanamgambo wa Al shabaab wanaoendelea kutatiza usalama katika kaunti ya Lamu tukio la karibu zaidi likiwa lile la siku ya Jumapili.

Haya yanajiri baada ya wanajeshi hao kufanikiwa kuwaua washukiwa 4 wa kundi hilo katika msitu wa Boni hapo jana na kunasa vifaa kadhaa vya kutekeleza mashambulizi kutoka kwa washukiwa hao.

Msemaji wa KDF David Obonyo amesema walifanikiwa kunasa bunduki 4 za AK-47,vilipuzi 3,bunduki 3 aina ya Pistol na gari lililoibiwa kutoka kwa maafisa wa polisi.

Obonyo amesema waliendesha oparesheni kali katika msitu huo uliowapelekea kukumbana na magaidi hao waliotaka kulichoma gari hilo lakini wakafanikiwa kuwaua mara moja.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287