GSU yapokea magari 30 ya kivita

 

yyyyyyyyy

Idara ya usalama ya kitengo cha GSU imepokea magari ya kisasa ya zana za kivita 30 al maaruf Armoured Personnel Carriers ambayo yanatarajiwa kusaidia kupigana na ugaidi.

Magari hayo yaliowasilishwa katika makao makuu ya GSU siku ya Jumamosi yamekabidhiwa idara hiyo na rais Uhuru Kenyatta katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa usalama nchini.

Serikali imesema magari hayo pia yatatumika na polisi ili kuwasaidia kukabiliana na visa vya uhalifu katika maeneo tofauti nchini.

Rais Uhuru amesema taifa la Kenya limejipanga vya kutosha kukabiliana na ugaidi na kwamba hawatokoma kusaka magaidi hao nchini Somalia ambapo wamechukua udhibiti wa miji tofauti.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287