Tunoi apinga madai ya kuhusika na hongo

 

image320

Jaji wa mahakama kuu Philip Tunoi amepinga vikali madai kuwa alipokea hongo ya shilingi milioni mia mbili kutoka kwa gavana wa kaunti ya Nairobi Evans Kidero.

Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya maalum inayomchunguza,amesema kuwa hakuna ushahidi wowote ambao unaonyesha alipokea hongo hiyo.

Kamati hiyo ya wanachama sita ikiongozwa na Margaret Kobia inamuda wa siku saba kuchunguza madai hayo na kisha kuwasilisha kwa ofisi ya jaji mkuu ili sheria kuchukua mkondo wake.

Jaji mkuu Willy Mutunga ameipa kamati hiyo muda wa siku saba kuwasilisha ripoti hiyo.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287