Serikali kueka mikakati kukomesha vita vya wanyama pori na binadamu

ffffff
Waziri wa mazingira Judy Wakhungu amesema kuwa serikali inaweka mikakati kuhakisha kuwa vita vya wanyama pori na binadamu vinamalizwa.
Akizungumza wakati wa sherehe ya kumtambulisha mkurugenzi mkuu mpya wa shirika la wanyama pori nchini kws Kitili Mbathi, Wakhungu amesema kuwa serikali ina nia ya kuweka fensi,Tsavo ambapo utata huo umeshuhudiwa zaidi.
Hata hivyo amesema kuwa zoezi la kuwalipa fidia wananchi waliouwawa na wanyapori litapewa kipaombele wakati watakapoa anza zoezi lakutowa fidia.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya KWS Richard Leakey amesema zoezi la uzungushaji wa fensi Tsavo linagharama kubwa huku akiomba wananchi walio katika maeneo yaliyoathirika kuiga mfano wa wakaazi wa Meru waliochangisha shilingi milioni 13 kwa ajili ya uzungushaji wa fensi.
Akizungumzia swala la sehemu ya pili ya ujenzi wa reli iliyo na kasi ya wastani  Leakey amesema majadiliano yangalia yanaendelea na bado uamuzi wa mwisho kuhusu njia ambayo gari hilo la moshi litakapopitia haijaafikiwa.
Aidha,Mbathi amesema kuwa atatembelea mashinani kufanya mjadala na washikadau na wafanyikazi wa KWS ili kuhakikisha kuwa shirika hilo linaimarika.
https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287