Rais aitaka AU kuangazia sheria za ushirikiano wao katika vita dhidi ya Al-Shabab

uuuh
Rais Uhuru Kenyatta ameutaka muungano wa Afrika kuangazia zaidi jukumu la muungano wa wanajeshi wa Afrika nchini Somalia AMISOM na kubadilisha sheria za ushirikiano wao katika vita dhidi ya Al Shabaab.
Rais Uhuru pia ameutaka muungano huo kutoa ufadhili zaidi ili wanajeshi hao waweze kukabiliana na kundi hilo angani , ardhini na majini.
Rais amesema haya wakati alipokuwa akihutubia baraza la usalama la muungano huo mjini Addis Ababa nchini Ethiopia na kusisitiza kuwa mbinu wanazotumia wanajeshi hao lazima zibadilike,ili kuwezesha wanajeshi wa Somalia kukabialiana na kundi la Al shabaab na kuwezesha serikali kudhibiti taifa lote la Somalia.

 

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287