Wamalwa akana madai kuwa mradi wa bwawa la Elgeyo Marakwet limekuwa likiongozwa na mzozo

 

download (1)

Sasa ni rasmi kuwa mradi wa ujenzi wa bwawa la maji katika eneo la Elgeyo Marakwet utakuwa chini ya halmashauri ya maendeleo katika eneo la Kerio Valley.

Hii ni baada ya kikao kati ya waziri wa maji na unyunyizaji wa mashamba Eugine Wamalwa kutatua mzozo ambao umekuwa ukikumba mradi huo kwa muda.

Akiongea baada ya kikao hicho kilichojumuisha viongozi mbalimbali kutoka eneo hilo, Wamalwa, amekanusha madai kuwa mradi huo umekuwa ukizongwa na mzozo akitaja swala hilo kama uvumi wa kupotosha umma.

Wakati huo huo, gavana wa kaunti ya Elgeyo Marakwet Alex Turgos pamoja na Seneta wa eneo hilo Kipchumba Murkomen wameitaka serikali kuhakikisha kuwa wote walioathirika na mradi huo wamefidiwa.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287