Dan Aloo aikashifu tume ya walimu TSC

Coast-Knut-NEC-member-Dan-Aloo-left-and-Mombasa-branch-KNUT-Secretary-general-Stephen-Ouma-during-a-press-briefing-1050x700

Katibu wa chama cha KNUT tawi la kilindini,Dan Aloo amekashifu tume ya walimu TSC kwa kudinda kuwalipa wanachama wa KNUT na vyama vya mikopo kwa walimu hali ambayo imeathiri shughuli za vyama hivyo.

Aloo pia amesema hali hiyo inaathiri uchumi wa nchi na kulemaza shuguli za vyama hivyo ambavyo ni ngao muhimu kwa maendeleo ya elimu nchini.

Katibu huyo pia amemtaka mkuu wa benki ya Kenya na waeka hazina kuishauri tume hiyo ya TSC kuhusu hali hiyo ya kutolipa muungano na vyama vya elimu inavyoathiri elimu nchini na hali ya kiuchumi kwa jumla.

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287