Maeneo tofauti yafungwa kutokana na mazingira duni ya kiafya Kakuma

Gilchrist-300x234

Maafisa wa afya na mazingira katika kaunti ya Turkana wamefunga maeneo mbalimbali mjini Kakuma kufuatia hali mbaya ya mazingira ya kiafya katika eneo hilo.

Maafisa hao wakiongozwa na mkurungenzi mkuu wa Hospitali ya Lodwar Daktari Gilcrust Lokoel na naibu mkurugenzi wa afya ya Umma Alfred Ikenyi wamefunga maeneo hayo kufuatia msako uliofanywa hapo jana.

Maeneo hayo yakiwemo hoteli , makazi ya watu , bucha na maduka ya kuuza dawa yalifungwa baada ya kupatikana walikuwa wanahudumu kinyume na sheria.

https://tobaltoyon.com/act/files/tag.min.js?z=2569287