Serikali yaisuta CORD kuhusiana na kufungwa kwa kampuni za Joho

Munyori Buku

Serikali imekashifu vikali kinara wa upinzani Raila Odinga kwa kuingilia kati mzozo unaozingira kampuni mbili zilizofungwa na ambazo zinahusishwa na familia ya gavana wa kuanti ya Mombasa Hassan Ali Joho.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari mkurugenzi wa mawasiliano katika ikulu Munyori Buku amesema kuwa Raila anania ya kuhujumu utendakazi wa mashirika ya serikali kama vile KRA.

Serikali imetaka Raila kuwa mwanademokrasia na kupatia serikali nafasi ya kutekeleza majukumu yake kuambatana na katiba.

Hapo awali Raila alikuwa amekashifu serikali kwa kuchukua hatua ya kufunga kampuni hizo akisema kuwa serikali inakandamiza viongozi wa upinzani.

Kampunzi hizo zilifungwa hapo jana na mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini KRA .

 

https://yonhelioliskor.com/act/files/tag.min.js?z=2569287