Kesi dhidi ya mshukiwa wa mauaji ya mwenyekiti wa CIPK kuskizwa mwezi ujao

Mombasa-Law-Court
Kusikizwa kwa kesi dhidi ya mshitakiwa Mohamed Sudi anayetuhumiwa kwa mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK, sheikh Mohamed Idriss,imeahirishwa hadi tarehe tano mwezi ujao.
Jaji Martin Muya amelazimika kuahirisha kesi hiyo baada ya mashahidi wawili ambao ni wakeze mshtakiwa kuanza kutofautiana mahakamani humo.
Jaji Muya ameagiza kuwa, mashahidi hao watatoa ushahidi wao mnamo tarehe tano ili waweze kukamilisha ukweli wao dhidi ya kesi hiyo.
Sudi anadaiwa kutekeleza mauwaji hayo mnamo tarehe 10 Juni 2014 katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa.
https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287