Taarifa kutoka mahakamani Mombasa

law-books_1

Mwanamume wa makamo anaetuhumiwa kwa kosa la mauaji katika eneo la Bangladesh wilayani Chanagamwe kaunti ya Mombasa amehukumiwa kifungo cha miaka 7 kwa kosa hilo katika mahakama kuu ya Mombasa.

Mshtakiwa Mourice Wamalwa amepewa adhabu hiyo na Jaji Martin Muya baada ya kumpata na hatia ya kuua bila kukusudia.

Shitaka dhidi yake ni kuwa mnamo tarehe 13 Julai mwaka wa 2013 katika eneo la Bangladesh wilayani Changamwe kaunti ya Mombasa kinyume cha sheria alimuua Kassim Bulimo.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287