Masomo yalemaa Lamu

articlesepaselect_KENYA_EDUCATION_SCHOOLS3.transformed

Huenda kaunti ya Lamu ikaandikisha matokeo duni ya mitihani ya kitaifa baada ya wanafunzi wengi kuonekana kusalia nyumbani kwa hofu ya mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa Alshabab.

Zaidi ya wanafunzi 400 wanadaiwa kutofika shuleni wiki ya 4 baada ya shule kufunguliwa muhula huu wa kwanza kutokana na sababu za utovu wa usalama uliokithiri katika kaunti hiyo.

Shule za msingi za Basuba, Milimani, Mangai, Mararani na Kiangwe hazijafunguliwa hadi sasa baada ya walimu wa shule hizo kutoroka kufuatia hofu ya mashambulizi huku tukio la karibu zaidi likiwa lile la siku ya Jumanne wiki hii ambapo maafisa 5 wa usalama wa kenya waliuawa.

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287