Chama cha wazazi nchini chafutiliwa mbali

431716

Waziri wa elimu Dr.Fred Matiang’i amefutilia mbali chama cha wazazi nchini kinachoongozwa na Musau Ndunda.

Kwenye taraifa yake,Matiang’i amesema chama hicho hakijaandikishwa katika sehemu yeyote ile katika wizara yake na kuwa hakitambuliki katika sheria za taifa.

Waziri ameagiza maafisa wa elimu kutoruhusu chama hicho kuitisha ada yeyote kutoka kwa wanafunzi kama ilivyokuwa hapo awali.

Chama hicho chini ya uongozi wa Musau Ndunda mara kwa mara kimejipata matatani kutokana na misimamo yake mikali.

https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287