Shinikizo latolewa kwa Waiguru kuwania Ugavana

ANNE-WAIGURU-HARAMBEE-HOUSE

Baadhi ya wanasiasa sasa wanamtaka aliyekuwa waziri wa ugatuzi Anne Waiguru kuwania kiti cha ugavana katika kaunti ya Nairobi.

Akizungumza jijini Nairobi aliyekuwa waziri wa mazingira kaunti ya Nairobi Evans Ondieki amesema kuwa ataunga mkono Waiguru kwani alionyesha utendakazi wake serikalini.

Kwa upande wake Waiguru amesema kuwa atashiriki mazungumzo na baadhi ya wadau kabla ya kutangaza kama atawani ugavana au la.

Waiguru alijiuzulu kama waziri wa ugatuzi baada ya wizara hiyo kukumbwa na kashfa kadhaa za ufisadi.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287