Rais aongoza ghafla ya kuwakumbuka wanajeshi waliouawa El Adde

2014623635390786619479333kenyan troops

Rais Uhuru Kenyatta,anaongoza  hafla ya kuwakumbuka wanajeshi wa KDF waliouawa na Alshabab katika shambulizi la El-adde nchini Somalia Juma lililopita.

Hafla hiyo inayofanyika katika kituo cha mafunzo ya kijeshi cha Moi Baracks mjini Eldoret, imehudhuriwa na marais Muhammad Buhari wa Nigeria na Hassan Sheikh Mahmoud wa Somalia pamoja na familia za waathiriwa wa tukio hilo.

Hafla hii inalenga kuwapa heshima wanajeshi hao waliouawa na wagambo wakati walipovamia kambi yao.

Haya yanajiri huku wanajeshi wa Kenya walioko nchini Somalia wakisemekana kukaribia mpaka wa Kenya, hatua iliyotajwa na serikali kuwa ya kuimarisha doria zao na sio kukwepa wanamgambo hao kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287