Hali ya taharuki yatanda Kilifi

crime-scene

Hali ya taharuki imetanda katika eneo la bundacho kaunti ya kilifi baada ya mzee kupatikana ameuawa na watu wasiojulikana.

Mwili wa Mzee huyo mwenye umri wa miaka 76 umepatikana nje ya nyumba yake mapema hii leo ukiwa na majeraha mabaya.

Mkuu wa polisi kaunti ya Kilifi Joseph Oleleina amesema uchunguzi umeanzishwa ili kuwatia mbaroni waliohusika na unyama huo.

Inadaiwa huenda kifo cha mzee huyo kinahusishwa na visa vya wazee katika kaunti ya Kilifi kuuwa kwa kigezo kuwa ni wachawi.

https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287