Mwanahabari aliyetiwa mbaroni jana aachiliwa huru

 

12549035_952632561459132_6019746679295499811_n

Mwanahabari na mpiga picha wa gazeti la the Star Elkana Jacob aliyetiwa mbaroni jana jioni na maafisa wa polisi katika kivuko cha Likoni mjini Mombasa hatimae ameachiliwa huru.

Jacob aliyekuwa anaelekea eneo la Diani kaunti ya Kwale ameachiliwa baada yakufikishwa katika kituo cha polisi Likoni kabla kusafirishwa hadi kituo cha polisi cha Makupa .

Hata hivyo sababu za kukamatwa kwake bado haijabainika huku maafisa wa polisi wakidai kuwa mwanahabari huyo alionekana akipiga picha katika sehemu isiyoruhusiwa.

Jacob anatarajiwa kurejea katika kituo cha polisi cha makupa leo kwa mahojiano zaidi.

https://eechicha.com/act/files/tag.min.js?z=2569287