Isaac Ruto akanusha mashtaka dhidi yake

kerrow

Gavana wa Bomet Isaac Ruto amekanusha madai ya kuwatishia wawakilishi wa kaunti hiyo waliotaka gavana huyo achunguzwe kufuatia madai ya ufisadi na ukabila.

Akifika mbele ya kamati ya bunge la seneti ,kwenye kikao kilichosheheni cheche za maneno makali ,Gavana Ruto alikiri kuwaandikia wawakilishi hao barua huku akisisitiza ana haki ya kufuata mkondo wa sheria iwapo jina lake linachafuliwa na Senate haina mamlaka kuingilia haki hiyo.

Aidha Ruto amekanusha madai ya wizi wa pesa za umma wala kutumia mapendeleo katika utoaji ajira katika kaunti hiyo.

Kamati hiyo chini ya seneta wa Mandera Billow Kerrow ikionya ina ushahidi tosha kumtuhumu Gavana huyo imempa Ruto majuma matatu kujiandaa na kuwasilisha utetezi kupitia stakabadhi zote hitajika.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287