Shule yafungwa kufuatia mgomo wa wanafunzi Kwale

ooooooooo

Shule ya sekondari ya Mnyenzeni huko Mazeras kaunti ya Kwale imefungwa.

Kulingana na taarifa moja kwenye mtandao wa kijamii Usimamizi wa shule hiyo umelazimika kuchukua hatua hiyo baada ya wanafunzi kushiriki mgomo.

Mmoja wa wazazi ameiambia radio salaam kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo amekuwa akiwahangaisha wanafunzi hata wenye deni dogo la karo.

Wanafunzi hao wamesikika wakisisitiza kuondolewa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.

https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287