Hitilafu ya umeme yasababisha mkanyagano na zaidi ya vijana 100 wa NYS kujeruhiwa

8e16da5181f14fea842a803b7de9119c

Zaidi ya vijana 100 wa shirika la huduma kwa vijana NYS wanauguza majeraha baada ya kukanyagana kufuatia hitilafu za umeme katika chuo cha mafunzo cha Gilgil.

Mkuu wa polisi bonde la ufa Gideon Amalla amesema kuwa hitilafu hizo zimesababishwa na mlipuko wa nyaya za umeme uliopelekea vijana hao kukanyagana walipokuwa wakijaribu kutoka katika eneo hilo.

Majeruhi wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja mjini Nakuru.

https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287