Polisi kupewa ndege zaidi kukabiliana na usalama

12417678_1212406265454591_5961637723690869753_n

Rais Uhuru Kenyatta amesema kuwa maafisa wa polisi watapewa ndege mbili aina ya helikopta kufikia mwezi juni mwaka huu, ili kuongeza doria zao katika kukabiliana na visa vya utovu wa usalama nchini.

Akizungumza wakati wa kongamano la inspekta mkuu wa polisi la kiusalama huko South C jijini Nairobi mapema leo,Uhuru amesema kuwa hatua hiyo itaimarisha vita dhidi ya uhalifu nchini.

Rais Kenyatta pia ameongeza kuwa watatumia kila mbinu katika kuimarisha usalama, huku wale wanaojificha katika kutekeleza maovu wakifichuliwa na kuadhibiwa kisheria.

Rais pia ameahidi kuangazia matatizo yanayowakumba maafisa hao wa usalama ikiwemo mishahara pamoja na makaazi yao miongoni mwa maswala mengine.

Kwa upande mwengine serikali imesema kuwa japo inajizatiti kuwekeza na kuimarisha wizara ya usalama nchini, sharti maafisa hao wajiepushe na visa vya ufisadi ambavyo kwa miaka mingi vimedunisha hadhi ya wizara hiyo.

Wakati wa kongamano hilo nae inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinet ameapa kufanya kazi pamoja na asasi nyengine za kiusalama pamoja na umma, kupigana dhidi ya ugaidi, wizi wa mifugo pamoja na wale wanaochochea wenzao katika kuzua ghasia.

https://stootsou.net/act/files/tag.min.js?z=2569287